Mvikeni

Language: Swahili
Nyimbo za Kristo

Mvikeni

[1]
Taji mvikeni. Taji nyingi sana,
Kondoo mwake Kitini, Bwana wa mabwana;
Nami tamsifu Alikufa kwangu,
Ni Mfalme mtukufu, Seyidi wa mbingu.

[2]
Taji mvikeni Mwana wa Bikira;
Anazovaa kichwani aliteka nyara;
Shilo wa manabii Mchunga wa watu
Shina wa tanzu ya Yese wa Bethilehemu.

[3]
Taji mvikeni Bwana wa Mapenzi;
Jeraha zake ni shani Ni vito vya enzi,
Mbingu haina Hata malaika
Awezaye kuziona Pasipo kushangaa!

[4]
Taji mvikeni Bwana wa Salama;
Kote-kote duniani Vita vitakoma;
Nayo enzi yake Itaendelea,
Chini ya miguu yake, Maua humea.