msaada wetu

Language: Swahili
Nyimbo za Kristo

msaada wetu

[1]
Mungu msaada wetu tangu miaka yote
Ndiwe tumaini letu la zamani zote.

[2]
Kivuli cha kiti chako ndio ngome yetu,
Watosha mkono wako ni ulinzi wetu.

[3]
Kwanza havijakuwepo nchi na milima,
Ndiwe Mungu; chini wako twakaa salama.

[4]
Na miaka elfu ni kama siku moja kwako;
Utatulinda daima , tu wenyeji wako.

[5]
Bwana msaada wetu tangu miaka yote,
Mlinzi wetu wa ngome, daima, milele.