Mkuu

Language: Swahili
Nyimbo za Kristo

Mkuu

[1]
Tabibu mku-u huyu, Yesu mwenye huruma:
Atuletaye faraja : Yesu mwokozi wetu.

Imbeni, Malaika Sifa za bwana wetu;
Jina la pekee kwetu, ni la Yesu Bwana.

[2]
Mwana kondo-o msifuni Mwokozi:
Hatia zote na dhambi Huziondoa Yesu.

[3]
Hakuna jina jingine Linalofa-a sifa:
A-u kutufurahisha, Isipo kuwa lake.

[4]
Naye atakapokuja Na utukufu wake,
Tutafurahi milele kuka-a kwake Bwana.