Mimi, Kristo

Language: Swahili
Nyimbo za Kristo

Mimi, Kristo

[1]
Si mimi, Kristo astahili sifa;
Si mimi, Kristo ajulikane;
Si mimi, Kristo katika maneno
Si mimi, Kristo kwa kila tendo.

[2]
Si mimi, Kristo kuponya huzuni;
Kristo pekee, kufuta machozi;
Si mimi, Kristo, kubeba mzigo
Si mimi, Kristo, kupunga hofu.

[3]
Kristo pekee, pasipo kujisifu;
Kristo pekee, na nisizungumze
Kristo pekee, na hakuna kiburi;
Kristo pekee, sifa yangu ife.

[4]
Kristo pekee, amhitaji atoe
Si mimi, kristo, kisima changu;
Kristo pekee, kwa mwili na kwa moyo.
Si mimi, Kristo, hata milele.