Mfalme

Language: Swahili
Nyimbo za Kristo

Mfalme

[1]
Mwumbaji, Mfalme
Vitu vyote vyako;
Ni kwa ukarimu wako
Ninabarikiwa,
Ni kwa ukarimu wako
Ninabarikiwa.

[2]
Uliyeniumba,
Nakutegemea;
Sina budi kuzisifu
Hisani zako kuu,
Sina budi kuzisifu
Hisani zako kuu.

[3]
Nitatoa nini?
Kwanza vyote vyako.
Upendo wako wadai
Moyo wa shukrani,
Upendo wako wadai
Moyo wa shukrani.

[4]
Nipewe neema,
Niwe na uwezo
Wakuishi kwako, Bwana:
Siku zangu, zako,
Wakuishi kwako, Bwana:
Siku zangu, zako.