Mbiu

Language: Swahili
Nyimbo za Kristo

Mbiu

[1]
Tumesikia mbiu: Yesu huokoa;
Utangazeni kote, Yesu Huokoa.
Tiini amri hiyo: nchimi baharini,
Enezeni mbiu hii: Yesu huokoa.

[2]
Imba nawe askari: Yesu huokoa;
Kwa nguvu ya kombozi, Yesu huokoa;
Imbeni wenye shida, unapounwa moyo,
Na kaburini imba: Yesu huokoa.

[3]
Mawimbini uenee. Yesu huokoa.
Wenye dhambi jueni: Yesu huokoa;
Visiwa na viimbe, vilindi itikeni,
Na nchi shangilie: Yesu huokoa.

[4]
Upepo utangaze: Yesu huokoa.
Mataifa ya shangaa: Yesu huokoa;
Milimani, bondeni, sauti isikike
Ya wimbo wa washindi: Yesu huokoa.