mapenzi makamilifu

[1]
Mungu u mapenzi mkamilifu Ypitayo fahamu za watu
Twanyenye kea sisi wapungufu, Wape baraka wapenzi wetu.

[2]
Ewe Mapenzi yasiyopimika Twawaombea kitini Mwako;
Wape mapenzi yasiyotindika, Waliooana mbele yako.

[3]
Ewe uhai, wewe u dhamana Ya imani na matumaini,
Wape kuvumilia hapa sana Wasiche maumivu mwishoni.

[4]
Wape furaha hiyo iwezayo Kutia nuru kwenye huzuni,
Wape amani hiyo itakwayo Katika matata duniani.

[5]
Waende mbele kusaidiana Maisha yao ulimwenguni;
Hata mwisho, ni kuja kwake Yesu, Wafurahi milele mbinguni.