litakasalo

Language: Swahili
Nyimbo za Kristo

litakasalo

[1]
Wimbi la damu ya Yesu Linatutakasa;
Aliumba kusudi Tupate uzima

Wimbi la damu naona naingia natakaswa!
Bwana asifiwe sana, Hutakasa, hutakaswa.

[2]
Damu inasema kwamba, Nasikia mvuto;
Inasema, moyo wangu Hutakaswa nayo.

[3]
Naondoka kutembea Kwa nuru ya mbingu;
Mavazi yamesafishwa; Moyoni ni Yesu.

[4]
Neema ni ya ajabu, Kutakaswa ndani!
Na kuwa naye Yesu tu, Aliye Mwokozi.