Lini Bwana

Language: Swahili
Nyimbo za Kristo

Lini Bwana

[1]
Mpaka lini Bwana
Utakaa mbali?
Kemetuchosha moyo
Kukawia hivi.
Utatujia lini,
Ili tu furahi
Katika ile nuru,
Kuja kutukufu?

[2]
Mpaka lini, Yesu,
Utaacha watu
Uliowakomboa
Wawe na mashaka?
Wachache waamini
Kwamba utarudi;
Wachache wa tayari
Bwana Kukulaki

[3]
Waamshe watu wako;
Tangaza kilio:
“Mwe watakatifu,
Bwana yu Karibu!”
Utatujia lini,
Ili tu furahi
Katika ile nuru,
Kuja kutukufu?