Langu Limeandikwa Je?

[1]
Siitafuti mali, wala utajiri;
Nataka kwa yakini nipate Mwokozi.
Chuoni mwa Ufalme, niambie Yesu,
Jina langu yakini limeandikwa, Je?

Limeandikwa, Je? Jina langu huko?
Kitabuni mbinguni, limeandikwa je?

[2]
Dhambi zangu ni nyingi, ni kama mchanga,
Lakini damu yako, Mwokozi, Yatosha;
Kwani umeahidi: zijapo nyekundu
Zitakuwa nyeupe ilivyo theluji.

[3]
Mji mzuri sana, wa majumba makuu,
Walipo malaika, mji bila ovu;
Wakakapo walio na mavazi safi,
Limeandikwa sasa, jina langu huko?