La Yesu Tamu

Language: Swahili
Nyimbo za Kristo

La Yesu Tamu

[1]
Jina lake Yesu tamu Tukilisikia,
Hutupoza, tena hamu Hutuondolea,

[2]
Roho iliyoumia Kwalo hutibika,
Chakula, njaani pia; Raha, tukichoka.

[3]
Jina hili ni msingi, Ngao, ngome, mwanba,
Kwa hili napata ungi, kwangu ni akiba.

[4]
Yesu, mchunga, Rafiki, Mwalimu, Kuhani,
Mwanzo, Mwisho, na Amina, Mali yangu yote!

[5]
Moyo wangu hauwezi kukusifu kweli;
Ila sifa zangu hizi, Bwana, zikubali.