la Yesu, salamu

Language: Swahili
Nyimbo za Kristo

la Yesu, salamu

[1]
Jina la Yesu, salamu! lisujudieni,
Ninyi mbinguni, hukumu, Na enzi mpeni.
Ninyi mbinguni, hukumu, Na enzi mpeni.

[2]
Enzi na apewe kwenu, watetea dini;
Mtukuzeni Bwana wenu, Na enzi mpeni.
Mtukuzeni Bwana wenu, Na enzi mpeni.

[3]
Enyi mbegu za rehema nanyi msifuni;
Mmeponywa kwa neema, Na enzi mpeni.
Mmeponywa kwa neema, Na enzi mpeni.

[4]
Wenye dhambi kumbukeni ya msalabani.
Kwa furaha msifuni, Na enzi mpeni.
Kwa furaha msifuni, Na enzi mpeni.

[5]
Kila mtu Duniani msujudieni,
Kote-kote msifuni, Na enzi mpeni.
Kote-kote msifuni, Na enzi mpeni.

[6]
Sisi na wao pamoja tu mumo sifani.
Milele sifa ni moja, ni “enzi mpeni”.
Milele sifa ni moja, ni “enzi mpeni”.