La Thamani

Language: Swahili
Nyimbo za Kristo

La Thamani

[1]
Jina lake Yesu tamu, Lihifadhi moyoni;
Litatufariji ndugu, Enda nalo po pote.

Jina la (Thamani) thamani, (thamani)
Tumai la dunia
Jina la thamani, (Jina la thamani-tamu!) thamani,
Furaha ya mbinguni.

[2]
Jina la Yesu lafaa Kama ngao vitani,
Majaribu yakisonga, Omba kwa jina hili.

[3]
Jina hili la thamani Linatufurahisha,
Anapotukaribisha, Na tunapomwimbia.

[4]
Mwisho wa safari yetu Tutakapomsujudu,
Jina hili tutasifu Furaha ya mbinguni.