La Rohoni Mwangu

[1]
Jua la rohoni mwangu, mpendwa Mwokozi wangu;
Usiku giza hapana, ukiwa karibu Bwana.

[2]
Nikipata usingizi, nijaze fikara hizi,
Ni tamu sana, nilale pendoni mwako milele.

[3]
Kaa nami, ewe Bwana, Usiku kama mchana,
Nisiishi mbali nawe; ni uhai kuwa nawe.

[4]
Kama mtoto mnyonge ameshawisha atange,
Mtafute Ewe Bwana, ujirudishie tena.

[5]
Wagonjwa wape amani, waneemeshe maskini,
Walio, Mtulizi, wape wote usingizi.

[6]
Asubuhi tutokapo, tukaribishe tulipo;
Twingiapo duniani tuwe mwako mkononi.