Kwangu

Language: Swahili
Nyimbo za Kristo

Kwangu

[1]
Yesu huita kwa upole mwingi, atwita wewe nami;
Moyoni mwetu hungoja, hukesha, Hukungojea wewe.

“Njoni kwangu, Mliochoka, njoni”
Yesu huita kwa upole mwingi, Akwita, “uje kwangu”

[2]
Atuombeapo usikawie, Hutuombea sisi;
Usidharau wema ma huruma, Huruma kwetu sisi.

[3]
Siku za maisha hupota hima, Hupita kwako, kwangu;
Usiku waja, kifo kinakuja, Huja kwako na kwangu.

[4]
Fikiri juu ya upendo wake, Upendo kwako, kwangu;
Dhambi zetu amekwisha samehe. Masamaha ni yetu.