kwa Yesu

Language: Swahili
Nyimbo za Kristo

kwa Yesu

[1]
Twende kwa Yesu mimi nawe, njia atuonya tuijue,
Imo chuoni; na mwenyewe, hapa asema njoo!

Na furaha tutaiona, myoyo iki takasa sana;
Kwako mwokozi, kuonana, na milele kukaa.

[2]
“Wana na waje,” atwambia furahini kwa kusikia;
Ndiye Mwokozi wetu hasa, na tumtii, njoni.

[3]
Wangojeani? Leo yupo: sakiza sana asemapo;
Huruma zake zitwitapo, ewe kijana, njoo.