kwa uzuri

Language: Swahili
Nyimbo za Kristo

kwa uzuri

[1]
Kumekucha kwa uzuri, Nafumbua macho;
Baba amenihifadhi, Ni wake mtoto.

[2]
Bwana niwe leo kutwa Ulinzini mwako;
Nisamehe dhambi, Niwe Mikononi mwako.

[3]
Roho wako anikae Moyoni daima;
Anitakase, nione Uso wako mwema.