Kuna Mvua Njema

Language: Swahili
Nyimbo za Kristo

Kuna Mvua Njema

[1]
Ati, kuna mvua njema yanya yenye neema;
Watu wanaona vyema Bwana, huninyeshei?

Na mimi? Na mimi? Bwana, huninyeshei?

[2]
Sinipite, Baba Mwema; dhambini nimezama:
Rehema ni za daima; Bwana, hunionyeshi?

[3]
Sinipite, Yesu Mwema; niwe nawe daima,
Natamani kukwandama: Bwana, hunichukui?

[4]
Sinipite, Roho Mwema, Mpaji wa uzima,
Nawe shahidi wa wema, Bwana wema hunipi?