Kitabu Chake

Language: Swahili
Nyimbo za Kristo

Kitabu Chake

[1]
Napenda kitabu chake, Kilichotoka mbinguni,
Barua kwangu ya Bwana Ujumbe wake wa upendo.

[2]
Humo ndani ya Kitabu Sura ya yesu naona
Karatasi zimekuwa, Wayo zake za Mwongozi.

[3]
Neno Lake ni maonju, Kubwe la asali tamu;
Natamani kuuonja Ule mkate wa uzima.

[4]
Mapenzi Yake Mwumbaji, Yanafunuliwa humo;
Hazina kuu ya hekima, Utajiri wa ajabu.

[5]
Mwangaza wa ulimwengu Angaza humo moyoni!
Uwe mwandamizi pote, Taa ya hatua zangu.