Kazi Zenu

Language: Swahili
Nyimbo za Kristo

Kazi Zenu

[1]
Fanyeni kazi zenu, usiku si mbali;
Kesheni saa zenu vumilieni;
Kwa Yesu tumikeni na hiyo Injili.
Sana wahubirini watu wa mbali.

[2]
Fanyeni kazi zenu giza ya songea;
Na wengi wenzi wenu wamo gizani,
Msipoteze moja dakika ni hizi;
Bwana atarejea mwisho wa kazi.

[3]
Fanyeni kazi zenu, hivi jua lachwa;
Wote walio kwenu apenda Mungu;
Na sisi tumjuaye na tuwafundishe
Ili Yesu ajaye tumfurahishe.