Kazi

Language: Swahili
Nyimbo za Kristo

Kazi

[1]
Usikatae Kazi yake Bwana; Ukae tayari kuifanya kazi;
Uende po pote Mungu akwitapo, Nawe utaona furaha kazini.

Njoo, We! Usiikatae; Njoo, We! Uifanye kazi;
Usikatae kazi yake Bwana, Ili hatimaye Usikatazwe juu.

[2]
Usikatae Kazi yake Bwana; kwa nini Kawia? Fanya kazi leo.
Mavuno meupe, Wachache Wavuni, Onyesha furaha Kwa kazi ya Bwana.

[3]
Usikatae Kazi yake Bwana, Kukataa pendo Kwako ni hatari.
Saa ya rehema, Yesu akiomba, Ziungame dhambi, Zifutwe mbinguni.