Juu Ya Mwamba

Language: Swahili
Nyimbo za Kristo

Juu Ya Mwamba

[1]
Tutajenga juu ya mwamba wa Yesu, Mwamba wa kale;
Tutavumilia kishindo tufani ivumapo.

Tutajenga juu, (Tutajenga juu ya mwamba mkuu)
Tutajinga juu, (Tutajenga juu ya mwanba mkuu)
Tuta jenga juu ya mwamba mkuu, juu yake Yesu.

[2]
Wengine hujenga katika Mchanga wa ulimwengu;
Wengine katika mawimbi ya anasa za dhambi.

[3]
Jenga nawe juu ya mwanba, Msingi pekee wa kweli:
Tumaini lake litadumu, tumai la wokovu.