Imara Mwambani

Language: Swahili
Nyimbo za Kristo

Imara Mwambani

[1]
Umtetee Mungu duniani ijapo pepo kali zavuma;
Mwanbani pekee pana nguvu Dhambi ikilemea.

Tusimame imara katika mwamba,
Mwamba wa Kristo pekee;
Ndipo salameni tutasimama
Kule kitini pa enzi.

[2]
Itetee Haki kwa bidii, kwa moyo mnyofu wa imani;
Mwambani pekee Utashinda wingi wa upotevu.

[3]
Itetee kweli, itadumu, ijapokawia itashinda;
Mwambani pekee pana raha yaishapo tufani.