Imara

Language: Swahili
Nyimbo za Kristo

Imara

[1]
Ahadi tamu kwa waamini, Tazama nakuja upesi sana.
Uwe imara, hatari kubwa: Ndugu usilale, bali ukeshe.

Uihifadhi imani yako,--Dunia mpya itatolewa
Njoo ingia furaha yangu; Taji zinangoja; Uwe imara.

[2]
Tatakesha na kutoa sala; Atakuja kama mwivi kwa wengi;
Ya kwamba yu karibu twajua, Ila hatujui ni siku gani.

[3]
Tunategemea Neno lake, Ambalo latangaza kuja kwake,
Tumaini letu ni ahadi: “naja karibuni, uwe imara.”