Huniongoza

Language: Swahili
Nyimbo za Kristo

Huniongoza

[1]
Njiani huniongoza. Yesu wangu, Mwokozi;
Rehema hatapunguza, Milele Kiongozi.
Ina raha kwandamana Duniani daima;
Nijaposumbuka sana, Yeye hutenda vyema,

[2]
Njiani huniongoza Hupunguza matata;
Nikiugua hupoza, Na njaani nashiba.
Lichokapo guu langu Nguvu zikapungua,
Jiwe lilo mbele yangu Hunibubujikia.

[3]
Njiani huniongoza Kwa pendo zilizo kuu,
Mwisho atanituliza Kwake Baba yangu juu.
Nikivikwa kutokufa, Nikae na Mwokozi,
Nitamsifu sana; sifa: “Kweli ni Kiongozi.”