Heri Kifungo

Language: Swahili
Nyimbo za Kristo

Heri Kifungo

[1]
Ni heri kifungo Kinachotufunga
Mioyo yetu kwa pendo Pendo la Kikristo

[2]
M-bele ya Baba Tunatoa sala;
Hofu, nia, masumbufu Yetu ni mamoja.

[3]
Tunavishiriki Matata na shida,
Na mara nyingi twatoa Chozi la fanaka.

[4]
Tunapoachana Moyoni twalia;
Lakini tutakutana M-wisho mbinguni.