Haja Nawe

Language: Swahili
Nyimbo za Kristo

Haja Nawe

[1]
Nina haja nawe kila saa;
Hawezi mwingine kunifaa.

Yesu nakuhitaji vivyo kila saa!
Niwezeshe Mwokozi, nkujia.

[2]
Nina haja nawe; kaa nami,
Na maonjo haya, hayaumi.

[3]
Nina haja nawe; kila hali,
Maisha ni bure, uli mbali.

[4]
Nina haja nawe, Nifundishe,
Na ahadi zako zifikishe.

[5]
Nina haja nawe; mweza yote,
Ni wako kabisa siku zote.