Giza

Language: Swahili
Nyimbo za Kristo

Giza

[1]
Mchana hauishi Mjini mzuri;
Mji hautapita; Na hapana giza.

Macho yatafutwa, Kifo hapana pale;
Hawahesabu siku, Na hapana giza.

[2]
Milango ni ya lulu, Mjini mzuri;
Dhahabu njia zake; Na hapana giza.

[3]
Milango haifungwi Mjini mzuri;
Mto ni wa uzima Na hapana giza.

[4]
Hawahitaji jua Mjini mzuri;
Mwana kondoo nuru; Na hapana giza.