Furaha Ya Moyo

Language: Swahili
Nyimbo za Kristo

Furaha Ya Moyo

[1]
Yesu, furaha ya moyo! Hazina ya pendo, na nuru.
Yote yatupendezayo, yasilinganishwe nawe.

[2]
Kweli yako ya daima, wawajibu wakwitao,
Ni siku zote u mwema kwao wakutafutao.

[3]
U mkate wa uzima, kupokea ni baraka,
Twanywa kwako u kisima roho zikiburidika.

[4]
Mwokozi twakutamani, kwako roho hutulia;
Twakushika kwa imani, nawe watubarikia.

[5]
Yesu, ndiwe kwetu mwanga, tufufahishe daima;
Giza ya dhanbi fukuza, uwe mwanga wa Uzima.