Ee Mlinzi

Language: Swahili
Nyimbo za Kristo

Ee Mlinzi

[1]
Niambie, Ee mlinzi, Umepambazuka je!
Utukufu wa Zayuni; Pana dalili zake?
Msafiri uondoke, Utazame mbinguni,
Kiunoni ujifunge, Ni kucha, alifajiri.

[2]
Mlinzi, inamurika nuru njiani mwako,
Dalili ya kuja kwake, Kwamba siku karibu;
Panda itakapolia Itawaamsha wafu,
Watakatifu wa Mungu, Kuwapa kutokufa.

[3]
Mlinzi, ione nuru Ya mwaka wa Sabato;
Sauti zina tangaza Ufalme ni karibu:
Msafiri ninaona mlima wa Zayuini,
Mji wa Yerusalemu nayo fahari yake.

[4]
Kwenye mji wa dhahabu Anaketi Mfalme
Katika kiti kizuri: Huku ana tawala.
Pana amani po pote, Mashamba husitawi;
Na ardhi ina rutuba; Mito ni mitulivu.