Dhambi Zangu

Language: Swahili
Nyimbo za Kristo

Dhambi Zangu

[1]
Sioshwi dhambi zangu bila damu yake Yesu,
Hapendezewi Mungu bila damu yake Yesu.

Hakuna kabisa dawa ya makosa
Ya Kututukasa ila damu yake Yesu.

[2]
La kunisafi sina ila damu yake Yesu,
Wala udhuru tena ila damu yake Yesu.

[3]
Sipati patanishwa bila damu yake Yesu,
Hukumu yanitisha, bila damu yake Yesu.

[4]
Sipati tumaini bila damu yake Yesu,
Wema wala amani bila damu yake Yesu.

[5]
Yashinda ulimwengu, iyo damu yake Yesu,
Na kutufikisha juu, iyo, damu yake Yesu.