Bwana Yesu

Language: Swahili
Nyimbo za Kristo

Bwana Yesu

[1]
Pengine ni saa ya kupambazuka, Mishale ya jua ipenyapo giza,
Kwamba atakuja Yesu mtukufu, Awapokee wake.

Bwana itakuwa lini Tutapoimba
“Anakuja, Bwana Yesu, Aleluya, Amin, Aleluya, Amin?”

[2]
Pengine mchana, pengine jioni, Pengine usiku wa manane, giza
Itatoweka kwa fahari akija, Awapokee wake.

[3]
Majeshi yake yataimba “Hosana,” Na watakatifu waliotukuzwa
Watamsifu kwa kuwa amekuja Awapokee wake.

[4]
Furaha tukiitwa pasipo kufa, Pasipo kuona maradhi, machozi;
Kuchukuliwa winguni kwa fahari Akija kwa watu wake.