Bwana, Nitume

Language: Swahili
Nyimbo za Kristo

Bwana, Nitume

[1]
Sauti ni yake Bwana, “Kwenda, nani tayari”
Mavuno yanakawia, Nani atayavuna?
Kwa kudumu amaita, Zawadi atatoa;
Nani atakayejibu “Nipo Bwana, nitume.”

[2]
Kana huwezi safari Hata Nchi za mbali,
Pana watu karibuni Wasio mjua Yesu;
Kama huwezi kusema Jinsi ya malaika,
Waweza kuutangazaUpendo wa mwokozi.

[3]
Ingawa huwezi kuwa Mkesha mlangoni,
Ukiwatolea watu Nafasi ya uzima;
Kwa sala na kwa sadaka Watoa msaada,
Kama Harun mwaminifu,Kuinua Mikono.

[4]
Roho za watu zikifa, Bwana akikuita,
Usiseme kwa uvivu, “Hakuna kazi kwangu.”
Kwa furaha anza kazi Ile akiyokupa,
Ukajibu mara moja “nipo Bwana, nitume.”