Biblia

Language: Swahili
Nyimbo za Kristo

Biblia

[1]
Nipe Biblia nyota ya furaha, wapate nuru wasafirio;
Hakuna la kuzuia amani,
Kwani Yesu alituokoa.

Nipe Biblia neno takatifu,
Nuru yake itaniongoza;
Sheria na ahadi na upendo,
Hata mwisho vitaendelea.

[2]
Nipe Biblia nihuzunikapo ikinijaza moyoni dhambi;
Nipe neno zuri la Bwana Yesu,
Nimwone Yesu Mwokozi wangu.

[3]
Nipe Biblia nipate kuona, hatari zilizo duniani;
Nuru ya neno lake Bwana Yesu,
Itaangaza njia ya kweli.

[4]
Nipe Biblia taa ya maisha; Mfariji tunapofiliwa;
Unionyeshe taa ya mbinguni,
Nione utukufu wa Bwana.