Bei

Language: Swahili
Nyimbo za Kristo

Bei

[1]
Yesu anasema, “Wewe huna nguvu
Kesha ukaombe, Na uje, Mwanangu.

Alilipa bei, Nawiwa naye;
Dhambi ilitia waa, aliiondoa.

[2]
Bwana, nimeona Uwezo wako tu
Waweza ‘takasa Mioyo michafu.

[3]
Sina kitu chema Kudai Neema,
Hivi nitafua Mavazi kwa damu.

[4]
Ninaposimama Juu ya mawingu,
Taji nitaweka Miguuni pa Yesu.