atukuzwe

Language: Swahili
Nyimbo za Kristo

atukuzwe

[1]
Mungu atukuzwe kwa mambo makuu,
Upendo wake alitupa Yesu,
Aliyejitoa maisha yake,
Tuwe nao uzima wa milele.

Msifu, msifu, dunia sikia;
Msifu, msifu watu wafurahi;
Na uje kwa Baba, kwa Yesu Mwana,
Ukamtukuze kwa mambo yote.

[2]
Wokovu kamili, zawadi kwetu,
Ahadi ya Mungu kwa ulimwengu;
Wanaomwamini na kuungama,
Mara moja wale husamehewa.

[3]
Alitufundisha mambo makuu,
Alihakikisha wokovu wetu;
Lakini zaidi. ajabu kubwa,
Yesu atarudi na tutamwona.