Ajapo

Language: Swahili
Nyimbo za Kristo

Ajapo

[1]
Mfalme wetu atuita tukae karamuni kwake;
Itakuwaje nasi kule Bwana akija?

Bwana ajapo, ndugu, Bwana ajapo!
Itakuwaje na sisi, Bwana akija?

[2]
Atavikwa vizuri sana,taji badala ya miiba;
Kweli tokeo la fahari Bwana ajapo.

[3]
Kwa fufaha awakubali wenye mavazi ya arusi;
Tu wa heri tukimridhisha Bwana ajapo.

[4]
Kutakuwako na utengo: watalia waliomwasi;
Cha kutisha kitambo kile Kristo ajapo!

[5]
Mfalme utupe neema sisi tunapokungojea
Tusiogope kukuona ujapo Bwana.