HALELUYA MSIFUNI

Language: Swahili
Nyimbo Za Umoja

HALELUYA MSIFUNI

[1]
Haleluya msifuni Bwana wa Mbingu
Sifuni na majeshi yake Mwokozi,
Heshima na apewe na utukufu
Popote duniani hata Mbinguni.

Milele kweli, milele kweli,
Milele kweli milele x2
Milele, milele, milele, milele x2
Popote duniani hata Mbinguni x2

[2]
Vijana wanaume na wanawali
Wazee na watoto shangilieni,
Kwa maana jina lake limetukuka,
Popote duniani hata Mbinguni.

[3]
Uzima wa milele ni kwa Mwokozi,
Nguvu zake Shetani zimeishashindwa,
Kwa maana ni Mwokozi alishakufa,
Wokovu duniani kwenda Mbinguni.