EE MWANADAMU

Language: Swahili
Nyimbo Za Umoja

EE MWANADAMU

[1]
Ee mwanadamu njoo kwa Yesu (Mwokozi wako)
Lisikieni neno lake m,
Upate wokovu kwa Bwana (uzima uko),
Yeye nuru ya ulimwengu,

Ewe mwanadamu, mtumikie Mungu
Wako m, usije ukaangamia (katika moto).
Siku ile inayokuja.

[2]
Je, wasemaje ndugu yangu (usiyetii)
Pokea neno lake Mungu m,
Ulitangaze wasikie (waje kwa Yesu)
Ameandalia makao.