HIVI NILIVYO UNITWAE

[1]
Nitwae hivi nilivyo, umemwaga damu yako,
Nawe ulivyoniita, Bwana Yesu, sasa naja.

[2]
Hivi nilivyo; langu kujiosha roho yangu;
Nisamehe dhambi zangu, Bwana Yesu, sasa naja.

[3]
Hivi nilivyo; sioni kamwe furaha moyoni,
Daima ni mashakani, Bwana Yesu, sasa naja.

[4]
Hivi nilivyo kipofu, maskini na mpungufu;
Wewe ndiwe u tajiri, Bwana Yesu, sasa naja.

[5]
Hivi nilivyo, mimi tu, Siwezi kujiokoa;
Na wewe hutanikataa, Bwana Yesu, sasa naja.

[6]
Hivi nilivyo; mapenzi yamenipa njia wazi;
Hali na mali sisazi, Bwana Yesu, sasa naja.

140