Song Lyrics

Kaa Nami

Lyrics

Font size:
Kaa nami ni usiku sana
Usiniache gizani bwana
Msaada wako haukomi
Nili pekee yangu, kaa nami

Siku zetu hazikawii kwisha
Sioni la kunifurahisha
Hakuna ambacho hakikomi
Usiye na mwisho, kaa nami

Nina haja nawe kila saa
Sina mwingine wa kunifaa
Mimi nitaongozwa na nani
Ila wewe bwana, kaa nami

Sichi neno uwapo karibu
Nipatalo lote si taabu?
Kifo na kaburi haviumi
nitashinda kwako, kaa nami

Nilalapo nikuone wewe
Gizani mwote nimulikie
Nuru za mbinguni hazikomi
Siku zangu zote kaa nami

Support My Songbooks

Help us expand our library and keep the music alive for everyone. Even a small donation goes a long way.

Buy me a coffeeBuy us a coffee