Song Lyrics

Amebarikiwa Anayetafuta Uso

Present

Lyrics

Font size:
Amebarikiwa anyemtumaini Jehova Mungu Baba X2
Atakulisha atakunywesha kweli atakuvisha X2
Jamii yako yote itabarikiwa kamwe hutapungukiwa X2

Omba Jehova Mungu Wako kwa moyo wako wote
atakupa ajaze moyo wako hatakuaibisha X2
Amebarikiwa anayetafuta uso wake Mungu Baba X2
Atakuonyesha mambo makubwa magumu usiyoyajua X2
Atakuponya atakufunulia ukweli na amani tele X2

Usichoke kutafuta uso wake Mungu Baba
atakupa chochote utakacho yeye ni mwaminifu
Bwana anasikia maombi ya wenye haki
atajibu Bwana hatawanyima kitu chochote

Amebarikiwa anayetafuta uso wake Mungu Baba X2
Atakufunika na mabawa yake Baba atakulinda X2
Atakuonyesha wokovu wake utaishi siku nyingi X2

Usichoke kutafuta uso wake Mungu Baba
atakupa chochote utakacho yeye ni mwaminifu
Bwana anasikia maombi ya wenye haki
atajibu Bwana hatawanyima kitu chochote X3

Support My Songbooks

Help us expand our library and keep the music alive for everyone. Even a small donation goes a long way.

Buy me a coffeeBuy us a coffee